Unawezaje kufanya michango kutumia CAMS?

Kufanya michango kwenda kwenye SACCOs yako kwa kutumia walleti yako ya mitandao ya simu sasa ni rahisi kwa kutumia CAMS.

  1. Ingia kwenye programu ya CAMS na bofya Michango yangu kwenye ukurasa wa mwanzo.
  2. Chagua aina ya akiba sahihi kutoka kwenye menyu. 
  3. Weka kiasi cha akiba. 
  4. Weka maoni yanayohusiana na mchango unaoweka (hii ni hiari).
  5. Bofya kitufe cha ‘Changia’.
  6. Chagua mtandao wako husika kisha bofya ‘Kubali’.
  7. Kiungo chenye ujumbe kitatumwa kwenye walleti yako ya mtandao wa simu. 
  8. Hakiki malipo na rudi kwenye programu ya CAMS.

Umemaliza! Mchango wako utaongezwa kwenye SACCOs yako.

Bonyeza kiungo kutazama video, kujua namna ya kutuma michango kwenye Saccos kwa kutumia simu kwenye CAMS.

https://www.youtube.com/watch?v=DQcHIph-kOM&t=50s