Nitawezaje kuomba mkopo?

Kama mwanachama wa SACCOs, unaweza kuomba mkopo kirahisi kwenye CAMS kwa kutumia simu yako ya mkononi. Baada ya idhinisho, kiasi chako cha mkopo kitahamishwa kwenda moja kwa moja kwenye walleti yako ya mtandao wa simu.Tazama video au fuata hatua zifuatazo kuomba mkopo kwenye SACCOs yako


  1. Ingia kwenye programu ya CAMS na bofya kwenye Mikopo yangu kwenye ukurasa wa mwanzo 
  2. Chagua aina sahihi ya mkopo unaotaka kutoka kwenye menyu
  3. Weka taarifa zinazohitajika kama kiasi cha mkopo, muda wa kulipa na jina la mdhamini nk. Kwa usahihi kwenye nyanja husika.
  4. Hakiki taarifa na bofya kwenye kitufe cha ‘Omba mkopo.

Umemaliza! Maombi ya mkopo yatakusanywa kwenye SACCOs yako. Utaona maombi yakiwa na hali ya ‘inasubiri’ 

Bonyeza kiungo kutazama video, kufahamu namna rahisi ya kutuma maombi ya mkopo kwenda kwenye Saccos kwa kutumia programu ya CAMS.
https://www.youtube.com/watch?v=DQcHIph-kOM&t=50s