Nitaingia vipi kwenye akaunti yangu ya CAMS?

Kama mwanachama wa SACCOs, unaweza kutumia taarifa ulizopewa na saccos yako kuingia kwenye akaunti yako. Tazama video au fuata hatua zifuatazo kuingia kwenye akaunti yako ya  CAMS.

  1. Fungua programu ya CAMS kwenye simu yako ya mkononi. 
  2. Kwenye ukurasa wa Kuingia, weka namba ya simu iliyounganishwa na akaunti yako. 
  3. Unaweza pia kutumia anuani ya barua pepe badala ya namba ya simu
  4. Weka nenosiri na bofya kitufe cha ‘Ingia’.   
  5. Chagua SACCOs unayotaka kuingia. 

Umemaliza! Sasa unaweza kutuma michango na kuomba mikopo kiurahisi kwa kutumia simu yako ya mkononi.

Video ya jinsi ya kuingia kwenye akaunti ya CAMS inapatikana pia kwenye ukurasa wetu wa YouTube; bonyeza tu kiungo hapa chini ili kuitazama.

https://www.youtube.com/watch?v=DQcHIph-kOM&t=50s